 |
| Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali, Swalehe Mohamed (mwenye fulana
nyeupe) aliyelazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es
Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai
29, 2016). |
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Said Mohamed (kushoto) na
Balitiamo Damian waliolazwa katika
taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake
aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwajulia hali, Isaya Sanga (katikati) na
Abasi Bushole waliolazwa katika taasisi
ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya
katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016). Kulia ni Mganga Mkuu wa
Taasisi hiyo, Dkt. Damian Msemo.
 |
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na ndugu za wagongwa waliolalazwa
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara
yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
|
 |
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa
katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara
yake aliyoifanya katika hospitali hiyo leo Ijumaa (Julai 29, 2016).
.............................
MAKAMU wa Rais, Mhe. Samia
Suluhu Hassan amefanya ziara yake ya kwanza katika Hospitali ya Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona wagonjwa
sambamba na kuangalia maendeleo ya
hospital hiyo.
Akiwa katika ziara hiyo
Mhe. Samia amebaini baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo
ya upungufu wa wauguzi na madaktari, uhaba wa mashine za mionzi, upungufu wa
vifaa tiba pamoja na upatikanaji wa dawa za Saratani kwa wagonjwa hao.
Amesema kuwa Serikali
itahakikisha inaongeza mashine mbili mpya za mionzi kwa ajili ya kupimia
wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya Saratani na kuahidi kupunguza deni la
MSD wanaloidai hospital hiyo ili wagonjwa waweze kupata dawa kwa gharama nafuu.
Mganga Mkuu wa Hospitali
hiyo Dk. Damian Msemo ameiomba Serikali
kuwekeza bajeti ya kutoshakatika hospital hiyo kwani inatoa huduma bure kwa
wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo hayo ambapo matibabu yake haa kwa upande wa
mashine ya mionzi hutumia gharama kubwa
Akifafanua utaratibu wa
kutibu wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa amesema kuwa hospitali hiyo
imeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa hao ambapo mgonjwa anayefika
mapema ndiye anayehudumiwa na kuongeza kuwa huwa wanatimu wagonjwa 160 kwa siku
kuanzia asubuhi hadi usiku licha ya uhaba wa vifaa tiba walionao”
“Hospitali hii tumeweka
utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika, mgonjwa anayefika mapema
ndiye anayehudumiwa kwanza
ukiacha wagonjwa wa dharula”
Amesema Dk. Msemo.
Amesema wagonjwa
wanaowafikia kutibiwa hospitalini hapo ni wengi ikilinganishwa na vifaa tiba
walivyonanvyo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu pale wanapokumbana na
changamoto mbalimbali.
Kwa upende wao baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata
matibabu wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taasisi hiyo kwa kujituma mbali
na uhaba wa waauguzi na changamoto za upatikanaji wa mashine za mionzi na dawa
kwa ajili ya kutibu matatizo hayo.
|