TRL YATOA RATIBA MPYA YA TRENI YA ABIRIA
Na Frank Wandiba Dar
Kampuni ya reli Tanzania(TRL) imefanya
mabadiliko ya muda wa treni ya abiria
kuelekea mikoa ya kigoma na mwanza kuanzia tarehe 2Agost 2016 treni
itaondoka saa Tisa (9) mchana badala ya saa 11 jioni muda wa sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar-es-salam, Meneja uhusiano wa (TRL)
MIDLADJY MAEZ amesema mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma za jiji kutoka kituo kikuu cha reli
Dar-es-salam kwenda Pugu ambayo inataanza kutoa huduma mapema siku ya jumatatu tarehe 1/8/2016.
Amesema mabadiliko hayo hayahusiani na ratiba
ya treni za abiria za kawaida ambazo uwa zinaondoka kila siku za jumanne na
ijumaa pamoja na treni za Deluxe zitahusika na mabadiliko hayo na zitaendelea na ratiba zake kama kawaida.
bw, MAEZ amebainisha kuwa uongozi wa kampuni Reli umetangaza mabadiliko haya kutokana na
sababu za kiusalama kwa kuepusha muingiliano unaoweza kutokea
na kupelekea kusababisha ajali.
Kwa upande wa safari za treni ya abiria kutoka
kigoma na mwanza hazitausika na
mabadiliko hayo na kuongeza kuwa kwa upande wa huduma ya treni ya jiji kwenda Pugu
itakuwa na vituo 10.
Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Pugu, Gongo la
mboto, FFU, Mombasa, Banana (njia ya kwenda stesheni) na karakata, Vingunguti, kamata
hadi kituo kikuu cha stesheni Dar-es-salam.
Aidha bwana MAEZ ameongeza kuwa safari za
treni ya jiji itakayokuwa inaenda Pugu itakuwa na awamu mbili asubuhi na
alasiri, ambapo treni ya kwanza itaondoka pugu 12:55 asubuhi kwa kufanya safari
tatu zitakazo mazika saa 5:50 asubuhi.
Kwa upande wa alasiri kutakuwa na safari tatu
pia ambapo treni itaondoka kituoni Dar-es-salaam saa 9:55 alasiri kwenda pugu na kuwasili 10:50 na safari ya mwisho
kuondoka Pugu saa 3:20 usiku kuja kituo kikuu cha Dar es salaam.




