Breaking News

Mhe Kimbita: Takribani Milioni 100 Zimetengwa Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Madarasa Katika Kata Ya Hananasifu

Diwani Wa Kata Ya Hananasifu Mhe. Ray Kimbita
Na Sala Mlawas
Takribani milioni 100 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari katika kata ya hananasifu iliyopo katika manispaa ya kinondoni jijini dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam diwani wa kata ya hananasifu Mhe. Ray kimbita alisema wamemuomba mkurugenzi wa manispaa awapatie viwanja kwa ajili ya wananchi waweze kupisha ujenzi wa shule hizo.

Alisema mpaka hivi sasa mkurugenzi wa maspaa ya kinondoni tayali amewapatia viwanja 10 vya kuwapatia wananchi ili waweze kuanza mchakato wa ujenzi wa madarasa hayo.

Aidha Mhe.KIMBITA aliongeza kuwa changamoto kubwa zinazozikabili shule za msingi za Hananasifu na Mkunguni ni ukosefu wa matundu ya vyoo sawa na na shule za sekondari hivyo basi atafanya jitihada aweze kutatua changamoto zinazokabili shule hizo.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Bi. Joyce Mwanga amewataka walimu waweke juhudi na ushirikiano ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Alisema pasipo kuwepo kwa jitihada za dhati za walimu hawatoweza kufaulisha wanafunzi kwa kasi kama walivyofaulisha mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kupatiwa zawadi kutokana na ufundishaji mzuri ambao ulipelekea wanafunzi kupata alama ya A Bw. Amfred Luanyo ambae mwalimu wa shule ya msingi ya Mkunguni  alisema zawadi hiyo imempa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mapinduzi katika taaluma.