Mtihani Wa Taifa Kitado Cha Pili Na Darasa La Nne Kuanza 13 Hadi 24 Mwezi Huu Tanzania Bara.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani Dkt. Charles Msonde.
Dar es salaam.
Jumla ya wanafunzi 521,855 wa kidato cha pili, na
wanafunzi 1,195970 wa darasa la nne kesho
wanatarajiwa kuanza Mtihani wa kitaifa wa upimaji kuanzia kesho tarehe 13 hadi 24 mwezi huu kwa upande wa Tanzania bara.
Akizungumza mapema
leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani Dkt. Charles Msonde
alisema kati ya wanafunzi 521,855 wa
kidato cha pili waliosajiliwa kufanya mtihani huo Wavulana ni 251,570 sawa na aslimia 48.21, Wasichana ni 270,285 sawa na aslimia 51.79.
Alisema kati ya wanafunzi
1,195970 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wavulana ni 592.005 sawa na asilimia 49.50, wasichana ni 603.965 sawa na aslimia 50.50.
“Idadi ya wanafunzi
waliosajiliwa kufanya upimaji huo imeongezeka ambapo mwaka jana waliosajiliwa kufanya
upimaji huo kwa kidato cha pili walikuwa 435,075
na darasa la nne walikuwa 1,054,191”
alisema Dkt. Msonde.
Aidha Dkt. Msonde aliongeza
kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kuandaa karatasi maalumu kwa
wanafunzi wasio Ona 56 na wale wenye
Uoni hafifu 330 ambao maandishi ya
karatasi zao za mmtihani ukuzwa.
“Maandalizi yote
yamekamilika pamoja na kusambazwa kwa kataratasi za maswali zitakazotumika kwa
ajili ya mtihani huo pamoja na nyaraka zote muhimu katika mikoa, Halmashauri
zote Tanzania bara” alisema Dkt. Msonde.



