Jengo La Kisasa La Upasuaji Hospitali Mwananyamala Lazinduliwa

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezindua
Jengo la Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es
salaam lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 420.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda katika picha ya
pamoja na watendaji wa hospitali ya Mwananyamala mara baada ya kuzindua jengo
jipya la upasuaji
Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa moja litasaidia kupunguza
idadi ya vifo mama na mtoto limepewa jina la HON. PAUL MAKONDA OBSTETRIC
THEATRE Kama sehemu ya kuenzi jitiada za Makonda katika kuboresha Sekta ya Afya
kwa kumtafuta mfadhili GSM Foundation aliekubali kujenga Jengo hilo bila
kutumia pesa ya Serikali.
Makonda aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo March
13 siku ambayo ndio aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa na sasa jengo limekamilika
likiwa na Vyumba Viwili vya Upasuaji vyenye uwezo wa kufanya upasuaji kwa
wakati mmoja na kuhudumia wagonjwa 20 kwa siku.
Makonda amesema kabla ya kujengwa kwa jengo hilo wagonjwa
walikuwa wakisongamana kusubiri kufanyiwa upasuaji kitendo kilichokuwa
kikisababisha maumivu makali na vifo vya mama na mtoto lakini kupitia jengo
hilo vifo vitapungua.
Makonda ameishukuru kampuni ya GSM Foundation kwa kufanikisha
Ujenzi wa jengo hilo ambapo inakadiriwa hospitali hiyo inapokea wagonjwa
kuanzia 1,500 hadi 2,000 kwa siku na miongoni wakiwa ni wajawazito wanaohitaji
huduma ya Upasuaji.
Makonda amesema hadi sasa zaidi ya Kinamama 55 wamejifungua
salama ndani ya jengo hilo na linaendelea kupokea wajawazito kila kukicha.
Baadhi ya wakiinamama waliofanyiwa upasuaji wamemshukuru
Makonda kuwajengea jengo hilo la upasuaji linalowawezesha madaktari kufanya
kazi yao pasipokuwa na usumbufu na wanafurahia kuona huduma za upasuaji
zikienda vema.
Viongozi waliohudhuriwa uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa wilaya
ya kinondoni, Mstahiki Meya wa Kinondoni,watendaji wa Afya na wananchi
wamempongeza Makonda kwa jitihada anazozifanya katika kuboresha sekta ya Afya
mkoani humo.



