Tume Ya Uchaguzi Yatangaza Majina 27 Ya Wagombea Udiwani

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imetoa majina 27 ya wagombea udiwani walioteuliwa na wasimamizi wasaidizi wa
uchaguzi kuwania nafasi hizo katika kata 10.
Uchaguzi mdogo katika kata hizo
utafanyika Februari 17,2018 kutokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu nyadhifa
zao na vifo.
Katika uteuzi huo wanaume
waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni 24 na wanawake ni watatu.
Taarifa iliyotolewa na NEC leo Ijumaa
Januari 26,2018 imesema wagombea wa kata nne waliteuliwa Januari 20 na wengine
wa kata sita waliteuliwa Januari 24,2018.
Wagombea waliojitokeza kuwania
udiwani katika kata ya Buhangaza iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera na vyama
vyao ni Jenitha Tibihenda (CCM), Nelson Makoti (Chadema) na Grayson Aniceth
(NCCR Mageuzi).
Katika Halmashauri ya Siha iliyoko
mkoani Kilimanjaro ambako kuna kata tatu zitakazofanya uchaguzi mdogo, wagombea
katika kata ya Gararagua ni Zakaria Lukumai (CCM) na Agness Lasway (Chadema).
Kata ya Donyomuruak wagombea ni Lwite Ndossi (CCM) na Daniel Molle (Chadema),
wakati katika kata ya Kashashi wagombea ni Suzan Natai (CCM) na Immanuel Saro
(Chadema).
Mkoani Mwanza ambako kuna kata mbili,
wagombea wa kata ya Kanbyelele iliyoko Halmashauri ya Misungwi ni Marco Yela
(ACT Wazalendo), Daniel Makoye (CCM) na George Mhoja (Chadema). Kata ya Isamilo
iliyoko wilayani Nyamagana wagombea ni Nyamasiriri Marwa (CCM), John Kisyeri
(Chadema), Hashim Ramadhan (CUF), Georgina Kibendegele (DP) na Ramadhani Mtoro
(UDP).
Kwenye kata ya Mitunguruni iliyoko
wilayani Singida wagombea ni Abdallah Mkoko (CCM), Manase Kijanga (Chadema) na
Abdallah Kinga (CUF).
Wagombea wa Kata ya Madanga iliyoko
wilayani Pangani mkoani Tanga ni Mohamed Abdallah (ACT Wazalendo), Athuman
Tunutu (CCM) na Swaibu Mwanyoka (CUF).
Mkoani Dodoma ambako pia kata mbili
zitafanya uchaguzi, kata ya Manzase iliyoko wilayani Chamwino wagombea ni Amos
Mloha (CCM), Alex Chalo (Chadema) na Ndahani Mazengo (Chaumma), wakati kata ya
Kimagai wilayani Mpwapwa mgombea ni Noah Lemto aliyepita bila kupingwa.



