Breaking News

Mtandao Wa Kijani Kibichi (MKIKITA) Wawapiga Msasa Wakulima Wa Zao La Papai Jijini Dar.

Image result for Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange
Mkurugenzi Mkuu wa shirikala Mtandao wa Kijani kibichi Tanzania (Mkikita), Dkt. Adam Ngamange.

Dar es salaam:
Watanzania wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea kwa kutegemea masoko ya kawaida badala yake wazalishe mazao katika mfumo wa mkataba.

Wito Huu umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa shirika lisilo la serikali la Mtandao wa Kijani kibichi (Mkikita)Tanzania Dkt. Adam Ngamange, katika wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la papai juu ya kilimo cha zao hilo salama.

"Umefika wakati sasa wakulima wabadilike waachane na kilimo cha kutegemea masoko ya holela holela kama Kariakoo na mengineyo watafute masoko rasmi kwa ajili ya kuongeza na kukuza kipato chao binafsi na Taifa," alisema Ngamange. 

Alisema ili wakulima wapate maendeleo wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kukutana na wataalamu wa kilimo mara kwa mara ili wawapatie ujuzi namna ya kuweza kuzalisha kwa wingi na namna ya kupata masoko.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bi. Elizabeth Msuya alisema kabla ya kupata mafunzo hayo alikuwa analima kwa mazoea bila kufuata kanuni za kilimo hasa kilimo biashara na kiwanda.

"Baada ya kupata mafunzo haya yamenisaidia kutambua namna bora ya kuendesha kilimo cha papai hivyo mategemea kubadili shughuli zangu za kilimo hasa zao la Papai, ambalo nilikuwa sijui kwamba anaweza kuuza nikapata fedha za kutosha kwa matumizi yangu na nyingine ya ziada," alisema Bi. Msuya.

Alisema ipo haja kwa wakulima kupewa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masoko ya mikataba na huria sambamba na mbinu za namna ya kutafuta masoko ya mazao yao.

Nae  mwanafunzi wa Chuo cha College of Agriculture and Natural Resources, Bi. Kogea Levi, ambaye ameshiriki mafunzo hayo ametoa wito kwa vijana kujikita katika kilimo hasa cha Zao la Papai kwa sababu kinalipa endapo mkulima atafuata ushauri wa wataalam.

"Ndoto yangu ni kuwa mkulima bora wa zao la Papai baada ya kuhitimu masomo tangu  baadae kwa sababu ni zao lisilohitaji investiment kubwa napenda kuwaondoa hofu vijana kuachana na dhana potofu kwamba kilimo in kazi ya watu wa vijijini," alisema Bi. Levi.