Picha: Mtoto Wa Miaka 4 Akutwa Jangwani Akitokea Syria Kwenda Jordan
Dunia imeamka na picha ya kusikitisha ya mtoto mwenye umri wa
miaka 4 ambaye anatoka Syria hadi Jordan.
Timu ya UNHCR imekumbana naye wakati akitembea peke yake bila
mlezi / mzazi jangwani kutoka Syria hadi Jordan.
Kitu pekee alichokuwa nacho katika mfuko wake wa karatasi ilikuwa mavazi ya mama na dada yake, ambao waliuawa Syria.
Picha ya pili inaonesha mtoto huyo akiwa miongoni mwa kundi kubwa la wakimbizi waliokatiza jangwani kuja Jordan kutokea Syria.
Source Mtandao





