Prof Lipumba: Wafanyabiasahara Watozwe Kodi Halisia
Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema
anaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli
katika mpango wa ukusanyaji kodi, huku akitaka utekelezaji huo uzingatie
uhalisia
Akisoma maazimio
ya kamati kuu iliyokutana mapema mwezi huu makao makuu ya chama hicho buguruni
jijini Dar es salaam, Prof. Lipumba alisema Baraza kuu la Chama cha Wananchi
CUF limeshauri mamlaka inayohusika na masuala ya ukusaji wa kodi kwa
wafanyabiashara wawe wanatoa makadirio mazuri ili kuweza kuwapa fursa wateja
zao kulipa kodi vizuri.
Alisema Baadhi ya makampuni na wafanyabiashara wanakadiriwa kodi kubwa
kuliko wanachouza na hatimaye kupelekea biashara zao kushindwa kujiendesha
matokeo yake zinafungwa”
"Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitika serikali ifanye
makadirio ya kodi ambayo yatakuwa yanazingatia hali halisi, Mamlaka ya kodi
isiwakamue wafanyabiashara mpaka biashara kufungwa na kusababisha kupata
hasara" Alisema Prof. Lipumba.
Aidha
Prof. Lipumba aliongeza kuwa chama cha wananchi tunaunga mkono katika ukusanyaji wa kodi lakini utekelezaji wake
uzingatie hali halisi, tusije tukawakamua watu wanaofanya biashara, hasa wenye
makampuni ambao ndio wanatoa ajira mpaka biashara na shughuli zao kupelekea
kuzifunga.
“Baraza kuu pia
limejadili uwepo wa malalamiko ya wananchi juu ya hali ya maisha kuwa magumu
kupitiliza hivyo kuiomba serikali iongeze mzunguko wa pesa ili kuweza kuinua
maisha ya watanzania wa hali ya chini.
Akizungumzia mpasuko wa chama hicho
kati yake na katibu mkuu wa chama hicho maalim seif alisema Baraza
kuu limesikitishwa na hatua ya Katibu mkuu ambaye alikuwa Mgombea wa Urais
kupitia Chama hicho kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015, kwa hatua yake ya kushindwa
kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi.
"Baraza
limesikitishwa maalim Seif kushindwa kufungua kesi mahakama kuu upande wa
Zanzibar sisi tunaamini endapo kesi ile tungeshinda basi chama chetu kingepata
Wakilishi sawa na Chama cha Mapinduzi CCM, jambo ambalo lingesaidia kuzuia
upitishwaji wa baadhi ya sheria kwenye Baraza la wakilishi" Alisema
Profesa Lipumba.
Aidha
Profesa Lipumba aliongeza kuwa Baraza kuu linasikitishwa na hatua ya Maalim
Seif kuendekeza kupandikiza migogoro na kuacha kufungua kesi ya msingi ya
kupinga uchaguzi , yeye anafungua kesi ya kuhoji uharali wa viongozi ndani ya
chama chetu.



