"Una Haki Ya Kulaumu Ili Upumue"-Nape Nnauye
Mbunge
wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Nape Nnauye
amefunguka na kudai kutohusika na kupanga mambo mbali mbali yanayoendelea
nchini baada ya kutuhumiwa kufanya hilo na mmoja wa raia.
Nape
Nnauye amefunguka hayo wakati akijibu moja ya hoja ya mtu aliyemtuhumu yeye
kama Mbunge wa CCM na kusema kiongozi huyo anajua na kuona haki za raia
zikivurugwa.
"Naamini
unaitwa Kusiluka, nimesoma lawama zako kwangu, una haki ya kulaumu ili upumue,
lakini kuna kikao nimeshiriki kupanga hayo unayonituhumu?! Nadhani kuwa mkweli kwa nafsi yako tuhuma hizo
ni nzito si sawa kuzisema bila kuwa na hakika, sihusiki na hayo usemayo na
nayalaani pia" Alidai Nape Nnauye
Nape
Nnauye aliwataka Watanzania kwa pamoja kuwasha mishumaa ya matumaini na hapo
ndipo mtu huyo alipoibuka mwananchi huyo na kusema kuwa kiongozi huyo yeye
anatambua na kujua kinachoendelea nchini sasa, jambo ambalo Nape
Nnauye amelikana na kusema hata yeye analaani kwa vitendo vinavyoendelea
nchini.




