IGP Sirro Apangua Makamanda Wa Polisi.. RPC Wa "Shambulizi La Aibu" Naye Kahamishwa

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon
Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi, Maulid Makabila kuwa Naibu Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai (D/DCI) Zanzibar, huku akifanya mabadiliko ya baadhi ya
makamanda wa polisi wa mikoa.
Kabla ya uteuzi huo, Makabila alikuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia
uhalifu makao makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana
Alhamisi Mei 17, 2018 na msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa imeeleza kuwa
katika mabadiliko hayo aliyekuwa DCI Zanzibar, Ramadhan Ng’anzi ameteuliwa kuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Charles Mkumbo
aliyehamishiwa makao makuu ya upelelezi, Dar es Salaam.
Aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa
Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali anakwenda kuwa kamanda wa
polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba. Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi
wa polisi, Thobias Sedoyeka aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es Salaam.
Kamanda Hassan Nassir Ali alizishika headlines za vyombo vya habari Tanzania Baada ya kusambaa kwa video aliyokuwa anazungumzia suala la kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wanaume wanao jikoholesha au hata kuwasumbua wanawake wenye makalio makubwa kwa madai kuwa hilo ni shambulizi la aibu
“Kamanda wa polisi mkoa
wa Kusini Unguja, Makarani Khamisi amehamishiwa makao makuu ya upelelezi
Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na kamishna msaidizi wa polisi, Suleiman
Hassan aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kaskazini Unguja,” anasema
Mwakalukwa katika taarifa hiyo.
Aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Hasina Ramadhani Taufiq anakuwa ofisa mnadhimu makao makuu ya
polisi Zanzibar na nafasi yake inachukuliwa na kamishna msaidizi, Haji Abdallah
Haji aliyekuwa ofisa mnadhimu Mkoa wa Mjini Magharibi.
Taarifa hiyo inaeleza mabadiliko hayo
ni ya kawaida yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.



