Inasemekana TECNO Kuja Na TECNO SPARK Kivyengine.
Kwa mara nyingine
tena inasemekana kampuni ya simu ya TECNO ipo mbioni kuachia simu mpya
ikidhaniwa kuwa ni muendelezo wa toleo la spark. Tetesi zimekua zikizaga kwa
wingi zaidi hasa mitandaoni na inasemekana simu hiyo kuingia sokoni tarehe
14/6/2018.
Na kulingana na
vuta nikuvute za kuhusiana na jina la simu pamoja na sifa zake wadau wameamua
kuipachika jina la utani kama TECNO SPARK 2, kwani toleo la spark ni moja kati
ya matoleo ya TECNO yenye ushawishi mkubwa sana hasa ukizingatia ubora wake wa
kamera pamoja na maumbo ya kuvutia.
Hivyo basi
inasemekana TECNO SPARK 2 ni zaidi ya spark yoyote maana safari hii inategemewa
kuja kivyengine ikiwa imeboreshwa zaidi kwa mfumo wa android. SPARK 2 inasemekana
kutumia mtandao wenye kasi zaidi ya ule wa 4G eti wanasema ukigusa tu umenasa.

Hadithi za
kuhusiana na simu inayosemekana ni TECNO SPARK 2 hazikuishia hapo kwani
inasemekana eneo kubwa la TECNO SPARK 2 lenye nchi kama 6.0 HD+ au zaidi ni
kioo kitupu chenye kuifanya simu kuwa na mvuto zaidi.
Na mvutano
unaonekana kuwa mkubwa zaidi katika upande wa ‘security’ kuna wanaosema iwe
isiwe lazima TECNO SPARK 2 itakuwa na ‘security’zaidi ya moja na moja wapo
ikiwa ni FACE ID na nyengine haijatambulika maana wadau wanadaiSPARK 2 kuwa
simu ya kwanza na aina hiyo ya ‘security’.

Tetesi zinadai
TECNO SPARK 2 itakuwa na aina mpya ya kionjo kwenye kamera ‘MIX FLASH’ ambacho
hupiga picha yenye kung’aa mithili ya kioo na inasemekana ufanyaji wake kazi ni
kama flashi 3 au zaidi ya tatu.Na endapo hizi tetesi zikawa na ukweli haswa
kuhusiana na hiyo MIX FLASHI ni ngumu kutabiri itakuwa na picha nzuri kiasi
gani kwani inasemekana SPARK 2 inapixel
za kamera 13+8 au zaidi.



