Kidato Cha 6 Kuanza Mtihani Wa Taifa Kesho

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta)
limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita
utakaoanza kesho Mei 7, 2018.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles
Msonde amesema leo Mei 6, 2018 kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari
amesema kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni
10,421.
Dk Msonde amesema mtihani utafanyika
sambamba na wa kozi ya ualimu ambao watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na
stashahada wamesajiliwa kuufanya.
"Maandalizi kwa ajili ya
mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu
vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk
Msonde



