Wakandarasi Dar Wamuunga Mkono Rc MAKONDA Kwa Kujenga Mitaro Bure.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda
Na Elisa Bin Shunda
Zaidi ya Kampuni 70 za ukandarasi zimejitolea kujenga mitaro
ya barabara mbalimbali za Dar es salaam Bure kama sehemu ya kuunga mkono jitiada za Mkuu wa
mkoa huo Mhe. Paul Makonda.
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kufanya ziara
usiku na mchana na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliotokana na ukosefu
wa mitaro ya maji na kuamua kuwashirikisha wakandarasi ambao walipokea kwa mikono miwili
ombi hilo.
RC Makonda amewaagiza wenyeviti wa mitaa
kuratibu idadi barabara zisizokuwa na mitaro kwenye mitaa yao kisha kupeleka
kwa Meneja wa TARURA Wilaya kwaajili ya kupatiwa kampuni itakayojenga mitaro
hiyo.
Aidha RC Makonda amezishukuru kampuni zilizojitolea
kujenga mitaro hiyo Bure jambo litakalosaidia kuokoa mabilion ya pesa za serikali.
Kwa upande wao wakandarasi wamesema wamejiandaa vizuri
kuanzia vifaa na wataalamu kwaajili ya ujenzi huo huku baadhi yao wakiwa tayari
wameanza ujenzi kwenye baadhi ya mitaa.







