Kikosi Cha Yanga Kilichokwenda Kenya Hiki Hapa

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Kenya kwa
ajili ya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup, inayotarajiwa kuanza June
03 hadi June 10 ikizihusisha timu nane huku 4 zikitoka Tanzania na 4 za Kenya.
Timu zote zinazoshiriki michuano hii ni zile zinazodhaminiwa
na kampuni ya Sportpesa ambapo kwa Tanzania ni Simba, Yanga, Singida United na
JKU ya Zanzibar.
Katika michuao hiyo inayoanza June 03 katika hatua
ya mtoano, Bingwa atajinyakulia kitita cha Milioni 68 pamoja na kupata nafasi
ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton inayoshiriki ligi kuu
nchini humo ya EPL, huku mchezo huo ukitarajiwa kufanyika kwenye dimba la
Goodison Park.
Hiki
hapa kikosi kamili kilichoondoka leo asubuhi na mapema:
Youthe Rostand Jehu, Ramadhan Kabwili, Hassan
Ramadhan Kessy, Buruan Yahaya Akilimali, Mwinyi Haji Ngwali, Pius Charles
Buswita, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Pato Ngonyani, Ibrahim Ajib Migomba na Maka
Edward.
Wengine ni Yohana Mkomola, Thabani Scara Kamusoko,
Matheo Anthony, Amissi Tambwe, Juma Hassan Mahadhi, Said Juma Makapu, Said
Mussa Bakari, Papy Kabamba ‘Tshishimbi’, Yussuf Mhilu na Raphael Daudi Loth



