SHEIKH JALALA AONGOZA MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA KIMATAIFA YA QUDS
Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala akizungumza mara baada ya matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza mara baada ya matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Naibu Katibu mkuu wa Idara ya Wanawake TIC Taifa, Bi. Fatma Mwiru akifafanua jambo katika Matembezi ya Amani ya siku ya kimataifa ya QUDS ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Dar es salaam:
Kiongozi mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala amewaongoza waislam na waumini wengine wa wa dini mbalimbali katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya kupinga manyanyaso, dhulma na mateso dhidi ya wapalestina yanayofanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Akizungumza na umma wa washiriki wa matembezi hayo shekh jalala amesema zaidi ya karne na karne sasa tangu dunia ianze kushuhudia mgogoro kati ya wa Israel na Palestina juu ya umiliki wa ardhi ya taifa la Palestina, pamoja na jitihada za kuutatua mgogoro huo ikiwemo kurekebisha mipaka ya ardhi kushindwa kufikia muafaka.
"Siku hii adhimu nyenye lengo la kuenzi na kupaza sauti juu ya amani, umoja na mshikamano kwa uislam na wasio waislam pamoja na kukumbuka madhila yanayoendelea duniani kote hususani katika ardhi ya Palestina " Alisema Sheikh Jalala.
Alisema siku Quds ni siku ambayo inawaleta pamoja waislam na wakristo pia ni siku ya kukumbuka madhila wanayoyapata taifa la palestina.
Sheikh Jalala aliongeza kuwa siku hii imekuwa ikiubili na kutangaza juu ya kuleta umoja kati ya waislam na wakristo , waislam na wayahudi kutokana na kukusanya dini zote pamoja na kupaza sauti kuimiza umoja, hasa katika ardhi ya Palestina katika mji wa Yerusalem mambapo ndio makao makuu ya dini zote mbili.
Nae Mwenyekiti wa chama chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kinachoendelea sasa mashariki ya kati sio jambo la kibinadamu hivyo nitoe rai kwa jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi.
"Asilimia 70 ya waanga wa mgogoro unaendelea mashariki ya kati kati ya israel na Palestina ni wanawake na watoto hivyo napenda kutoa rai kwa jumuia ya kimataifa kuingilia kati kupatia ufumbuzi mgogoro huo" Alisema Prof. Lipumba
Matembezi ya siku ya Quds mwaka huu 2024 yamebeba ujumbe wa "QUDS BILA VITA NI ISHARA YA AMANI"













