Breaking News

WAZIRI SILAA AHIMIZA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

Dar es salaam - Waziri wa Mawasiliano na teknolojia, mheshimiwa Jerry Slaa ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuenzi na kulinda tunu yetu ya amani, umoja na mshikamano wetu katika kujenga nchi. 

Wito huo ameutoa leo April 20, 2025 katika tamasha kubwa la mtoko wa pasaka lilofanyika katika ukumbi wa super dome masaki

Alisema nchi yetu tumejaaliwa tunu hii adhimu hivyo tunao wajibu wote kuhakikisha kuwa tunaienzi na kudumisha amani, umoja na mshikamano wetu kwani linaendeleza upendo na haki katika kujenga nchi. 

"Ukiangalia hasa katika mitandao ya kijamii utaona adha ambayo wanaipata wananchi ambao nchi zao zina machafuko na hakika utaona kuwa amani tuliyonayo si ya kuichezea". Alisema Waziri Silaa.

Alisema kupitia Tamasha la Mtoko wa Pasaka ambalo litaenda sambamba na maombi ya kuliombea Taifa litawaleta pamoja wasanii wa muziki wa injili akiwemo Rose Muhando, Christina Shusho, Solomon Mukubwa, na wengine wanatarajiwa kuhudumu katika tamasha hilo ambalo pia linaenda 

Tamasha la mwaka huu limebeba kauli mbiu isemayo 'Kwa maombi utashinda'ni kielelezo cha jitihada za kuendelea kuitunza amani tuliyonayo".