Breaking News

ALEX MSAMA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

Dar es Salaam, Juni 29, 2025 – Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, leo amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Msama alipokea fomu hiyo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala kutoka kwa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Chief Sylvester Yaredi.

Hatua hiyo inaashiria dhamira ya Msama kuwania nafasi ya uongozi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.