TANZANIA KUWA MWENYEJI WA TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII kw6a AFRIKA NA BAHARI YA HINDI
Dar es salaam - Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za 32 za kimataifa za utalii kwa ukanda wa Afrika na bahari ya hindi ambapo wageni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo June 11 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii(TTB) Ephraim Mafuru amesema lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa wadau wa utalii Duniani
Aidha amesema wadau wa sekta ya utalii katika mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuchangamkia fursa za mkutano huo katika kuwahudumia wageni
Amesema kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa wenyeji wa tuzo hizo kwa nchi za afrika kumetokana na ushindi wa nchi katika tuzo zilizopita Kwan iliongoza kwa kuwa na tuzo 5 tofauti na nchi zingine za afrika.
"Uwepo wa tuzo hizi nchini ni jitihada za Rais Dk Samia Suluhu hassan tunapaswa tumpongeze Tuzo kama hizi ziliwahi kufanyika miaka ya nyuma ambapo hazikuwa kwa ukubwa kama ilivyo sasa",amesema Mafuru
Aidha amesema Shughuli kama hii mwaka jana 2024 ilifanyika Mombasa kenya Tanzania ilishinda tuzo tano ambapo bodi bora ya utalii yaAfrika ilichukua TTB,kivutio bora cha utalii Afrika ilikuwa mlima Kilimanjaro, hifadhi ya taifa bora Afrika ilikuwa Serengeti, kivutio bora cha safari Duniani sasa mafanikio haya hayaji tu hivi hivi ni kazi kubwa imefanyika ikiongozwa na Rais wetu",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na utalii zitashiriki ambapo washiriki 38 kutoka sekta bifasi na 12 kutoka Serikalini watashiriki.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli ya Johari Rotana ambae ndio 'Host' wa tuzo hizo Ahmed Said amesema wao kama hoteli wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahudumia vyema wageni wote watakaofika kwenye tuzo hizo.
Naye,Mkurugenzi wa Masoko kutoka hospitali ya Shifaa Victoria Tarimo amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma za kimataifa katika kuwahudumia wageni hao ambao watapata changamoto za kiafya wakati wa tuzo hizo.
"Sisi tumejipanga vizuri na tunavifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya kuwahudumia na tutakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha tunawapa huduma nzuri kwani tunavifaa vya kisasa na wataalam wa kutosha lakini pia tutakuwa na gari la wagonjwa kwa ajili ya dharura",amesema.
Amesema Hospitali imejipanga kusapoti agenda ya Rais Dk Samia ya Tiba utalii kwa vitendo.
Tuzo hizo zilianIshwa mwaka 1993 lengo likiwa kutambua mchango wa wadau walipo katika sekta ya utalii katika maeneo mbalimbali Duniani ambapo sasa zinatarajiwa kufanyika june 26,2025 katika hotel ya Johari rotana jijini Dar es salaam ambapo hoteli hiyo pamoja na hospitali ya shifaa ndio watakaohudumia watu katika Tuzo hizo.








