WAKILI MALOGOI ACHUKUA FOMU GEITA KUPAMBANA NA MUSUKUMA
Geita — Wakili Malogoi amejiweka rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kwa kuchukua fomu ya kugombea Jimbo la Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo inaashiria dhamira yake ya dhati kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, huku akilenga kuwatumikia wananchi wa Geita kwa uadilifu, uwajibikaji na uwakilishi makini. Wakili Malogoi, ambaye tayari ana historia ya ushiriki katika siasa, anarudi tena katika ulingo wa kisiasa akiwa na matumaini ya kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo ya jimbo hilo.
Hii ni sehemu ya mchakato wa ndani ya chama wa kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Kwa sasa, Jimbo la Geita linawakilishwa na Mbunge Joseph Kasheku Musukuma kupitia CCM.




