ADC YAMPITISHA WILSON ELIAS KUPEPERUSHA BENDERA YA URAIS TANZANIA BARA, HAMAD RASHID ZANZIBAR
Dar es Salaam — Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimemchagua rasmi Wilson Elias kuwa mgombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Katika mkutano mkuu maalumu wa chama hicho, wajumbe walimuidhinisha Elias kwa kura ya ndiyo na hapana, kufuatia kutokuwepo kwa mgombea mwingine aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo.
Kwa upande wa Zanzibar, wajumbe hao pia walimchagua aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Hamad Rashid Mohamed, kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ADC. Naye alipita bila kupingwa baada ya kukosa mpinzani wa ndani ya chama.
Kupitishwa kwa wagombea hao wawili kunafungua rasmi ukurasa wa maandalizi ya ADC kuelekea uchaguzi mkuu, chama kikilenga kushindana katika nafasi kuu za uongozi wa nchi.





