AKILI UNDE KUJADILIWA TANZANIA, SAMBAMBA NA UZINDUZI WA MFUMO MAALUM WA AI KULINDA MAADILI KUZINDULIWA
Dar es salaam - Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kupitia Tume ya TEHAMA, imeanzisha Jukwaa la Tanzania la Akili Bandia (AI) lenye lengo la kuwakutanisha watumiaji wa teknolojia hiyo kutoka sekta mbalimbali, ili kujadili fursa, changamoto na maadili katika matumizi ya AI nchini.
Jukwaa hilo limeundwa kama sehemu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa Tanzania hainyimwi nafasi katika mapinduzi ya teknolojia ya kidijitali, huku kipaumbele kikiwa ni matumizi salama na yenye kuzingatia maadili ya kitaifa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 16, 2025 jijini dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa
Tume ya Tehama, Dk. Nkundwe M. Mwasaga amesema Jukwaa hilo litatumika kama njia ya kuhamasisha mjadala mpana kuhusu matumizi ya AI katika nyanja kama elimu, afya, kilimo, biashara, na utawala, pamoja na kuangazia namna ya kuweka mifumo itakayodhibiti matumizi yasiyofaa ya teknolojia hiyo.
Aidha, juhudi zimeanza kufanyika kuandaa mfumo wa kitaifa wa udhibiti wa AI utakaolenga kulinda maadili, haki za binadamu na usalama wa kidijitali, sambamba na kuhakikisha matumizi ya teknolojia hiyo yanachochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
Kwa hatua hii, Tanzania inajiunga na mataifa mengine duniani yanayoangazia umuhimu wa kuwa na miongozo mahsusi kuhusu AI, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inatumika kwa manufaa ya wote bila kuathiri maadili ya kijamii.
Jukwaa hilo litafanyia Julai 29 na 29 mwaka huu katikaukumbi wa superdome masaki jijini Dar es salaam




