NEEMA MCHAU ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA VITI MAALUM MANISPAA YA ILALA
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto, Neema Mchau, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Ilala.
Akikabidhiwa fomu hiyo leo Julai 1, 2025 na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Rosemary Mwakisalu, Neema alieleza dhamira yake ya kulitumikia taifa kwa bidii kupitia nafasi hiyo.
Neema aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa, akisisitiza kuwa CCM ni chama kinachotoa fursa kwa wanawake na kinaongozwa na misingi ya demokrasia.
"Ni wakati wa wanawake kusimama imara na kuchukua nafasi katika uongozi. Tusikubali kurudi nyuma, wakati ni sasa," alisema Neema.
Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea viti maalum unaendelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala.





