Breaking News

RC MAKONGORO NYERERE AIBUKA MSHINDI WA PROMOSHENI YA WORLD CUP YA CRDB TEMBO CARD VISA

Dar es Salaam – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, ameibuka mshindi katika droo kubwa ya kampeni ya FIFA World Cup 2026 “Fainali Ndiyo Mpango na Tembo Card Visa” iliyoendeshwa na CRDB Bank mapema leo Mei 12, 2026.

Droo hiyo ilifanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kurushwa mubashara, ambapo washindi waliopatikana kupitia matumizi ya Tembo Card Visa walipigiwa simu na kupewa taarifa za ushindi wao.

Kupitia droo hiyo, Makongoro Nyerere amejishindia safari ya kwenda nchini Canada kushuhudia fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026.

CRDB imeendelea na droo yake ya pili ya kampeni hiyo inayolenga kuwapeleka washindi nchini Marekani, Canada na Mexico kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia 2026, yatakayoshirikisha mataifa mbalimbali duniani.

Kampeni hiyo inayojulikana kama “Fainali Ndiyo Mpango na Tembo Card Visa” pia imepata washindi wengine watatu waliozawadiwa TV Janja nchi 85 pamoja na washindi watatu waliojishindia safari ya kwenda Canada.