Breaking News

DKT. MARIA PETRO AINGIA FAINALI YA WAZO BUNIFU, ALENGA KUBORESHA HUDUMA ZA TRA

Na Mwandishi Wetu - Daktari wa binadamu, Dkt. Maria Petro kutoka mkoani Kigoma, ni miongoni mwa wabunifu 60 waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Wazo Bunifu, linalolenga kupata mawazo bunifu yatakayochangia kuboresha huduma za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Dkt. Maria amefika mbele ya Kamati Huru ya Wazo Bunifu leo, Oktoba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwasilisha na kutetea wazo lake kupitia mahojiano ya ana kwa ana.

Amesema ana matumaini kuwa wazo lake likichaguliwa kuwa mshindi na kutekelezwa, litasaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa walipakodi na kuboresha mahusiano kati ya TRA na jamii kwa ujumla.

Utekelezaji wa wazo hilo unatarajiwa kuchangia katika kuboresha uzoefu wa walipakodi wanapopata huduma kutoka TRA, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya mamlaka hiyo na wananchi.