Breaking News

ESAP MINING YATWAA TUZO TATU MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

GEITA — Afisa Utawala na Mawasiliano wa ESAP Mining Services Limited, Shabani Sadiki, amesema kampuni hiyo imepokea tuzo tatu katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.

Sadiki amesema tuzo hizo ni pamoja na tuzo ya Mdhamini Maalum wa Maonesho, tuzo ya kampuni bora katika huduma za uchorongaji migodini (drilling), pamoja na tuzo ya mshindi wa pili katika kampuni za uchimbaji madini.

Amesema tuzo hizo ni chachu kwa ESAP Mining Services Limited kuendelea kuongeza juhudi, ubunifu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma kwenye sekta ya madini.

Aidha, Sadiki ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka sheria, sera na kanuni zinazosisitiza Local Content na ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini, akisema hatua hizo zimeendelea kuwapa wazawa fursa ya kushiriki na kuwekeza katika sekta hiyo.

Amesema mafanikio hayo yamewezekana kupitia ushirikiano kati ya uongozi na wafanyakazi wa ESAP pamoja na wadau mbalimbali wanaofanya kazi na kampuni hiyo, akiwataja Nyanza Mining, Buckreef, STAMIGOLD, Shanta Mining, wachimbaji wadogo wa Tanzanite na wadau wengine.

ESAP Mining Services Limited imeendelea kutoa huduma za uchorongaji na huduma nyingine katika sekta ya madini, huku ikiendelea kushirikiana na kampuni za migodi na wachimbaji wadogo nchini.