POLISI DAR YATOA ONYO KWA WANAOPANGA VURUGU NOVEMBA 6
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linafuatilia taarifa za kundi la watu wanaodaiwa kuhamasishana ndani na nje ya mkoa huo kuingia jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanya fujo, vurugu na hujuma mbalimbali Novemba 6, 2026.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo, amesema jeshi hilo halitavumilia viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani na litachukua hatua za haraka kwa mujibu wa sheria dhidi ya mtu au kundi lolote litakalobainika kujihusisha na mipango hiyo.
Aidha, Murilo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia kampeni ya Ongea na Kamanda, inayolenga kujadili changamoto za kiusalama katika maeneo yao na kutafuta suluhisho kwa pamoja.
Pia, amewataka wananchi kuheshimu taratibu zilizowekwa na Mahakama katika kufuatilia mashauri mbalimbali yanayoendelea mahakamani.




