Video: Miaka Kumi Na Tano Ya The Foundation For Civil Society, Mkurugenzi Aeleza Mipango Mipya.
Shirika lisolo la kiserikali ya The Foundation For Civil
society linalojihusisha na kujenga uwezo wa asasi za kiraia nchini Tanzania
pamoja na Kutoa ruzuku kwa asasi hizo linatimiza miaka kumi na Tano tangu
kuannzishwa kwake na kuanza kufanya kazi.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii Mkurugenzi
mtendaji wa shirika hilo lenye ofisi zake Jijini Dar es salaam Ndugu Francis
Kiwanga alisema kuwa kwa miaka kumi na tano ya uwepo wake nchini wamefanikiwa
kufanya kazi na Asasi zisizopungua elfu tano nchini ikiwa ni mafanikio makubwa
kwa shirika hilo lililojumuisha asasi tofauti.
Nakupa nafasi ya kumsikiliza mkurugenzi wa shirika hilo
akieleza kwa undani, kazi walizozifanya kwamiaka 15, changamoto walizopitia nma
mipango ya kuendelea kuihudumia jamii kwa sasa.



