Kitengo cha Vijana NCCR Mageuzi Chatangaza Vipaumbele Vyake Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020
Mwenyekiti wa Kitengo cha vijana NCCR Mageuzi Bw. Nicolas Clinton
akisoma maadhimio ya kikao cha siku mbili kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)kuelekea uchaguzi mkuu 2020 makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Uongozi wa KITENGO CHA VIJANA TAIFA umefanya kikao cha siku
mbili tarehe 31/07 na 1/08 kujadili mustakabali wa Vijana kwa miaka mitano ijayo, vipaumbele
vyetu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 na mapendekezo ya mahitaji ya Vijana ya Miaka mitano
(Agenda za Vijana 2020 – 2025). Na hii imetokana na kuona kama taifa tumekosa dira ya vijana ya
pamoja kuelekea kutekeleza Dira ya Maendeleo 2025.
Tukiwa ni vijana ambao tunaamini kwa zaidi ya 65% ya watanzania wote ni sisi vijana, na amabao
ndio chachu ya maendeleo ya taifa letu.
Tukizingatia kuwa mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambapo wananchi watapata fursa ya
kuchagua viongozi wao katika nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani kwa Amani ili mama Tanzania
abaki salama baada ya uchaguzi.
Tukiamini kuwa sisi vijana tunaweza kutekeleza majukumu yetu na kuwa sehemu muhimu katika
kuleta maendeleo, badala ya kuwa wapokeaji na wanufaika wa malengo na mikakati iliyoandaliwa
pasipo na ushiriki wetu ulio thabiti,
Tunatambua kuwa sekta isiyo rasmi ina jukumu kubwa katika kutoa fursa za ajira na mapato kwa
vijana nchini Tanzania,
Tunatambua kuwa kunasekta muhimu ambazo zinazogusa vijana wengi zaidi lakini zimegubikwa
na changamoto mbali mbali.
Mfano
1. kilimo bado ni shughuli ya msingi nchini Tanzania, chanzo kikuu cha chakula kwa wananchi na
chanzo cha mapato kwa mtu mmoja mmoja na katika ngazi ya kitaifa,
2. Ajira, idadi kubwa ya vijana kukosa ajira,uwezo mdogo wa kujiajiri na hivyo kuwa tegemezi
3. Afya janga la ufikiaji duni wa huduma bora za afya kwa vijana hasa maeneo ya vijijini,
4. Miundombinu rafiki kwa vijana, uhitaji wa miundombinu na rasilimali zinazohitajika katika
kutatua changamoto za afya na za kielimu kwa vijana nchini Tanzania,
Ikizingatiwa kuwa mwaka 2025 ni mwaka ambao Tanzania imejipangia kutekeleza Dira ya
Maendeleo 2025.
Naibu katibu mkuu Bara NCCR Mageuzi Bi. Ndilonkeye Kifua akitoa maelezo katika mkutano na waandishi (hawapo pichani) makao makuu ya makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.
AJENDA ZA VIJANA 2020 - 2025 AMBAZO KITENGO CHA VIJANA NCCRMAGEUZI KITAISIMAMIA.
1. Ajira kwa Vijana
Uchumi haujatoa fursa za kutosha za ajira kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa,
ambao wanachukua zaidi ya 65% ya watanzania wote. Utafiti umeonyesha kuwa
ukosefu wa ajira kwa vijana ni zaidi ya 50% haswa katika maeneo yote nchini.
Yafuatayo ni masuala ambayo yanahitaji kushughulikiwa na serikali pamoja na
wadau wa maendeleo ya vijana.
Utekelezaji wa sheria na sera madhubuti ambazo ni nzuri kukuza ukuaji wa ajira
kwa vijana,
Ushuru unapaswa kupunguzwa ili kuunda/kukuza mtaji wa wajasiliamali vijana
Utoaji wa ruzuku kwa wakulima wa kilimo cha biashara haswa kwa wajasiriamali
vijana,
Ujasiriamali unapaswa kujumuishwa katika mtaala wa mfumo wa elimu yetu.
Uanzishwaji wa mfuko wa uwezeshaji wa vijana chini ya Baraza la Vijana huru la
kitaifa.
Uboreshaji wa usafirishaji na mawasiliano ili vijana wanaojishughilisha na kilimo
cha biashara cha kisasa kupata urahisi wa masoko.katika bidhaa za kilimo.
2. Elimu Bora
Imerekodiwa kwamba idadi ya watoto waliojiandikisha kujiumga na elimu ya
msingi imeongezeka kwa miaka 10 iliyopita kufikia 90%, hii pia imesababisha
kuongezeka kwa idadi ya vijana katika sekta ya elimu kutoka msingi hadi kiwango
cha vyuo vikuu.
Kinyume chake sekta ya elimu inakabiliwa na changamoto kama
uhaba wa walimu, vifaa vya kufundishia, ujuzi duni na maarifa, majengo duni ya
shule za msingi na sekondari ambayo yamepitwa na wakati hivyo majengo mengi
ya shule zetu hayasanifu mazingira ya sasa ya uchumi wa kati na hali ya
teknologia duniani, hivyo Kujifunza kwa vitendo kunapaswa kushughulikiwa/ kuwa
kipaumbele hasa katika elimu ya mafuzo ya ufundi na serikali lazima iakikishe
ubunifu wa vijana katika teknologia hasa kwenye kilimo, viwanda, na artificial
intelligence ili kukuza ushiriki wa vijana katika uchumi wa nchi yetu, kundi hili ni
muhumu katika mageuzi ya kiuchumu Tanzania.
Kuboresha mazingira ya kusomea/kujifunzia kwa wanafunzi na pia kuboresha
mazingira ya walimu kufundishia.
Mtaala unapaswa kuonesha/kuakisi mabadiliko ya kiteknologia, kijamii, kiuchumi
na kisiasa.
kiswahili kinapaswa kutumiwa kama lugha kuu na njia ya kufundishia.katika
mfumo wetu wa elimu.
Vitabu vigi vinapaswa kutangazwa na kukaguliwa kila wakati na usimamizi wa
mitihani shuleni na vyuoni inapaswa kuboreshwa zaidi.
3. Huduma Bora za Afya
Vijana ndio kundi lililoathiriwa zaidi katika jamii iliyo na magonjwa tofauti kama magonjwa
yanayoambukizwa kwa njia ya zinaa.na mengine mengi.
Makamu Mwemyekiti Bara NCCR Mageuzi, Bw. Lutufyo Mwambara akielezea jambo katika mkutano na waandishi (hawapo pichani) makao makuu ya makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam
Tunapendekeza Mfuko wa bima ya afya ya kitaifa unapaswa kuwachukua vijana katika sekta
isiyo rasmi,
kuboresha miundombinu ya afya kama kuongeza dawa, na vifaa tiba hasa maeneo ya vijijini.
kuboresha mazingira/hali ya kufanya kazi katika sekta ya afya, kupambana na rushwa katika
sekta ya afya na kuimarisha zaidi uwajibikaji wa kada hiyo.
4. Utawala Bora na Uwajibikaji
KITENGO cha Vijana NCCR-Mageuzi kinashauri Uhuru wa vyombo vya habari
unapaswa kuzingatiwa na kulindwa ikiwa pamoja na kuzingatia uhuru wa kisiasa
pamoja na kuwaachia Huru au kuwapa dhamana viongozi wa BARAZA LA VIJANA
CHADEMA ambao wanashikiliwa kwa muda mrefu sana mpaka sasa,Hivyo KITENGO
cha vijana tunaziomba mamlaka zinazohusika kuwaachia Katibu Mkuu wa BAVICHA
na viongozi wote wa baraza la Vijana wanaoshikiliwa na jeshi la polisi Nchini. kulinda
haki za binadamu, kuakikisha raia wanawawajibisha viongozi wao na TAKUKURU
kuwa tasisi huru katika kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi na MAHAKAMA
YA UFISADI inapaswa kupewa nguvu zaidi ya kukabiliana na vindo hivyo kwenye
jamii na muhimu zaidi ni ajenda ya kudumu ya NCCR-Mageuzi ya mabadiliko ya katiba
ya wananchi.
5. Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana kwenye vyombo vya maamuzi.
Uundwaji wa Baraza la Vijana huru la kitaifa na utekelezaji wake, kuhakikisha mfumo
mzuri wa ujumuishaji wa vijana kwenye vyombo vya maamuzi kuanzia ngazi za kijiji
hadi Taifa, kuhakikisha kuna mwakilishi wa vijana kutoka Balaza la Vijana katika
vyombo vya maamzi vya ngazi zote.
6. Vijana na Rasilimali za Taifa
Kuweka mfumo wa uwazi kuruhusu umma kujua mikataba na makubaliano yote yaliyotolewa
kati ya serikali na wawekezaji tofauti juu ya rasilimali asili. Kuweka sera inayoongoza na
kuelekeza wawekezaji wa kimataifa kuajiri asilimia 75% ya watanzania wa ndani. Kuanzisha
viwanda vikubwa na vya kati kwa kuongeza thamani kwenye bidhaa za maliasili. Mapitio ya
Sheria ya Ardhi ya Kijiji na sheria zingine kuwaruhusu raia wamiliki ardhi kwa ajili ya kilimo na
uwekezaji katika maliasili. Uboreshaji wa mitaala ya elimu kuzingatia kuingizwa kwa moduli
kwenye rasilimali asili pamoja na rasilimali za madini, mafuta na gesi ili kuakisi na kulinda
nguvu kubwa ya vijana kushiriki kwenye ujenzi wa uvhumi imara na mkubwa kwa taifa.
7. Sekta ya Sanaa na Michezo
Kuongeza idadi ya vyuo vya Sanaa katika kanda mbalimbali za nchi, sheria sahihi
zinazolinda haki za wasanii zinapaswa kutekelezwa, uboreshaji wa misingi ya
utendaji/usimamizi, utoaji wa ruzuku kwa wasanii na wabunifu.
Uanzishwaji wa shule maalum za Michezo za kikanda kama ilivyo shule maalum za
vipaji kitaaluma mfano tabora boys, pugu boys, mzumbe na nyinginezo.
8. Vijana wenye ulemavu
KITENGO cha Vijana kinapendekeza Kuanzishwa na uboreshaji wa taasisi ya ujifunzaji
kwa vijana wenye ulemavu, kuhakikisha uwakilishi wa vijana wenye ulemavu katika
mihimili ya kufanya maamuzi, uboreshaji wa miundombinu ndani ya jamii iliyojumuishi
kwa vijana wenye ulemavu, kuelimisha jamii juu ya ulemavu ili kuondokana na
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano na Umma NCCR Mageuzi, Bw. Kitenya Luty akifafanua jambo katika mkutano na waandishi (hawapo pichani) makao makuu ya makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam
unyanyapaa na uwezeshaji wa jamii. ya vijana wenye ulemavu kiuchumi na utoaji wa
mikopo isiyo na riba na ujuzi wa ujasiriamali.
Uwepo wa mfuko maalum wa uwezeshaji kiuchumi (Mikopo isiyokuwa na riba) kwa
vijana wenye ulemavu.Selikali itazame kuwa ni bora vijana wenye ulemavu kupewa
ruzuku ili waweze kushiriki katika maendeleo ya taifa kuliko hivi sasa kundi hili
linakabiliwa na changamoto lukuki.
9. Usawa wa Kijinsia
NCCR-Mageuzi inazingatia sana masuala ya usawa kijinsia katika sera, katiba
na kununi zake ili kuakikisha tuna jamii inayoshirikisha makundi yote kwenye
jamii. Kuhakikisha fursa sawa kwa wasichana na wavulana kuamua juu ya afya
zao, miili yao, jukumu la kijinsia na utambulisho wao. Kuhakikisha upatikanaji wa
afya ya uzazi kwa vijana wa kike na kiume bila kujali umri wake, hali ya ndoa na
kiwango chake cha elimu. kuakikisha utoaji wa huduma salama za afya ya uzazi,
upangaji wa familia, nafasi za uzazi wa mpango, Kuhakikisha maamuzi huru
kuhusu masuala ya ndoa yatahakikishwa kwa vijana wa kike na wa kiume.
Kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na
ubakaji.
10. Vijana na Diplomasia na Uongozi bora
NCCR-Mageuzi inaandaa vijana wazalendo na wenye kuguswa na matatizo ya Taifa letu,
Vijana watatumika kama chombo cha kutafiti na kushauri serikali kwa njia ya Amani
katika masuala ya kijamii, kiuchumi, kiasiasa na katika masuala ya sayansi na
tecknolojia. Vile vile tunawasihi Vijna kushiriki katika shughuli za ubunifu na
kuakikisha serikali inaweka kipaumbele kwa vijana wabunifu katika Nyanja zote.
NCCR-Mageuzi pia inandaa vijana viongozi wenye mtazamo wa kimageuzi na hivyo
vijana wenye kutaka kufanya siasa zenye masuala na hoja mahali sahihi ni NCCR-
Mageuzi, itikadi ya UTU inalenga kuwaunaganisha vijana na makundi mengine yote
nchini kushiriki siasa ambazo zinakisi utamaduni wa Tanzania na maitaji ya Nchi.
Mtazamo wetu kundi hili la vijana ni kubwa mno lakini limeachwa mbali na mifumo
katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuchimi na hasa kwenye sekta pia ya
teknologia ambayo kwa sasa inaweza kuajili vijana wengi sana.
HITIMISHO
Ndugu waandishi wa habari, huu utakuwa mwelekeo wa KITENGO cha Vijana katika
masaula ya vijana na tutawaomba wagombea wetu katika nafasi zote kuhakikisha
Ajenda ya vijana inasukumwa ili kuleta matokea chanya kwa vijana wote Nchini.
KITENGO cha Vijana kitaendelea kutoa mwelekeo wa vijana na kuongoza katika
kufanya utafiti ili kuishauri serikali kutimiza wajibu wake kwa vijana. Tutaendelea pia
kusisitiza kufanya siasa za UTU na kulinda heshima ya Amani na utulivu wa NCHI
YETU.
Vijana ni rsmali kuu ya Taifa na hivyo nguvu ya vijana itumike katika ujenzi wa
Uchumi wa Nchi yetu. Elimu inayotolewa Nchini, serikali ihakikishe inakuwa ni ya ujuzi
zaidi ili kuakisi mabadiliko ya teknologia na sayansi duniani, Taifa letu sasa limefikia
uchumi wa kati ni muhimu serikali kuhakikisha inawekeza kwa VIJANA hasa kwenye
eneo la elimu ya mafunzo ya ufundi ili Vijana wengi washiriki kwenye ujenzi imara wa
uchumi wetu.
Mungu ibariki Africa,
Mungu ibariki Tanzania,
PAMOJA TUTASHINDA.







