MEYA KUMBILAMOTO: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA TAASISI BINAFSI KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI
Mstahiki Meya wa Jiji Dar es salaam Omary Kumbilamoto akikata utepe kufungua hosptali mpya ya Royal Polyclinic Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa Jiji Dar es salaam Omary Kumbilamoto akizungumzaa katika hafla ya ufunguzi wa hosptali mpya ya Royal Polyclinic Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa Jiji Dar es salaam Omary Kumbilamoto akiwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Bw. Ahmed Mohamed mara baada ya ufunguzi wa hosptali mpya ya Royal Polyclinic Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam:
Mstahiki Meya wa Jiji Dar es salaam Omary Kumbilamoto ameomba taasisi binafsi kuunga mkono Serikali kwa juhudu zao za kuendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kusaidia kuwapunguzia kutembea mwendo mrefu kufuata huduma
Ombi hilo amelitoa leo Dar es salaam katika hafla ya Ufunguzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic Mnazi Mmoja ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita kipaumbele chake ni kuboresha afya ya wananchi hivyo hospitali hiyo itatoa huduma kwa wananchi wote pasipo kubagua rangi, jinsia, dini, wala kabila
Sanjari na hayo amesema taasisi binafsi ikiwemo, taasisi za kiserikali dini, mtu binafsi zimekuwa zikisaidia jamii katika masula mbalimbali ikiwemo kusaidia Makundi Maalumu kwa kutoa Misaada huduma za kiafya hivyo Serikali anatambua juhudi zao na iko tayari kuwasaidia changamoto zinazowakabili kwani baadhi yao hawana maeneo ya kujenga hospitali wamepangisha majengo ambayo hata eneo la kuegesha magari hakuna.
“Sisi kama Jiji la Dar es Salaam tunafarijika kwa kuzindua hospitali hii hapa kwani itaipunguzia mzigo hospitali yetu ya Mnazi Mmoja. Tunashukuru kwa jambo hili ambalo mmelifanya,” Alisema Mstahiki Meya Kumbilamoto.
Alosema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani amekuwa akifanya jitihada kubwa kuboresha huduma za afya na tayari ameshatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Ujenzi wa vituo vikubwa vya Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambavyo vitajengwa maeneo ya Mchikichini na Kiwalani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Royal Polyclinic, Bw. Ahmed Mohamed amesema katika kila mafanikio changamoto hazikosekani kwani hapo walipo wametoka mbali walianza na dispensari na wafanyakazi wawili na hadi hapo jambo la kumshukuru Mungu kwa kufikia hospitali na kuzalisha ajira zaidi ya 40
Mohamed aliongeza kuwa tayali wameanza kitoka huduma Zanzibar na kwamba katika Kituo hicho cha Dar es Salaam wamejipanga vilivyo katika kuwahudumia wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa ufanisi mkubwa kupitia madaktari
“Kituo hiki tumejipanga kuwahudumia wananchi Kwa ufanisi mkubwa kupitia Madaktari bingwa huduma ya Meno, maabara, Ultra Sound, Physiotherapy, dawa na vifaa Tiba kwa gharama fedha taslimu na bima ya afya hivyo wananchi wote tunawajali” alisema Bw. Ahmed






