Breaking News

MPANGO WA WANAUME KUSHUDIA WAKE ZAO WAKIJIFUNGUA WAMKOSHA RAIS SAMIA

Rais Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na mpango wa hospitali ya CCBRT kujenga vyumba binafsi kwa ajili ya wajawazito kuvitumia kujifungua ambavyo vinaruhusu mzazi anayejifungua kuwa na mzazi mwenzake (Mume wake) au ndugu yake ambapo amesema kuwa wakati wa kujifungua Mwanamke uhitaji faraja.

"Nimefurahishwa na mpango wa kuwa na vyumba nane binafsi kwa ajili ya kujifugua, vinavyoruhusu mzazi kuwa na mwenza au ndugu yake, hakuna wakati wa faraja kama wakati wa kujifungua, ukiwa na mtu wako pembeni ambaye anakusaidia kukupooza" -Rais Samia Suluhu Hassan

"Kuna vitoto vidogo kabisa miaka minne, mitano, sita wanapokelewa hapa wana Fistula, ndugu zangu tuone tatizo hili la ubakaji kwa kiasi kikubwa tunalifumbia macho huko kwenye jamii hatulisemi, hatuwapeleki kunakohusika wanaokosea" -Rais Samia Suluhu Hassan, ameyasema wakati wa uzinduzi wa jengo Uziduzi Jengo huduma kwa Mama na Mtoto kwenye hospitali ya CCBRT  leo  Julai 5, 2022