TAMASHA KUBWA LA ONGALA MUSIC FESTIVAL KUFANYIKA AGOUST 4 JIJINI DAR
Mratibu wa tamasha la Ongala Music Festival, bw. Thomas Ongala akiongea katika mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia Agosti 4 hadi 6 jijini Dar es salaam.
Mratibu wa tamasha hilo Bi Aziza Ongala akifafana jambo katika mkutano na waandiahi wa habari kuelekea tamasha kubwa la kumuenzi mwanamziki Remmy Ongala lilopewa jina la Ongala Music Festival litakalofanyika kuanzia Agosti 4 hadi 6 jijini Dar es salaam.
Na Timothy Marko Dar es Salaam
Katika kuhamasisha Muziki wa kitanzania Mtoto wa Mwanamuziki wa zamani wa Dance Remmy Ongala, Thomas Ongala ameandaa Tamasha la Muziki litakalo fanyika tarehe 4 hadi 6 Agosti 2022 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa tamasha hilo bw. Thomas Ongala amesema lengo la kuandaa Tamasha Hilo ni kuenzi Muziki wa baba yake Mzazi.
"Baba kashaweka Mizizi katika Muziki, sisi tumeandaa Dance ngoma na vionjo vya live Muziki". Alisema Thomas Ongala .
Ongala Aliongeza kuwa lengo la kufanyika kwa Tamasha hilo ni kuendeleza Muziki wa Msanii huyo tumejifunza kuwa Mtu anaweza kuishi kupitia Muziki kwa kujisajili katika taasisi za Cosota na Basata .
Alisema Ongala Music festival ulianza 2008 na huu ni msimu wa nne ambapo katika awamu zote tamasha hilo limekuwa likifanyika katika jiji la Dar es Salaam.
"Nawapongeza Basata na Chuo cha sanaa Bagamoyo (TASUBA) katika kufanikisha Tamasha hili". Alisema Thomas Ongala.
Kwa upande wake mratibu mwenza wa tamasha hilo bi Aziza Ongala amesema Tamasha Hilo linatarajia kujumuisha Bendi 60 na kiingilio Cha Tamasha Hilo ni shilingi Tsh 10,000.





