Breaking News

JUMIKITA YALAANI UDHALILISHAJI NA MATUSI KWA VIONGOZI MITANDAONI

Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) imelaani tabia mpya na mbaya iliyoanza kujitokeza nchini ya kutukana na kuwadhalilisha viongozi mitandaoni.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jumuiya hiyo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti hiyo, Shaaban Matwebe amesema tabia hiyo ni mbaya na chafu yenye kulenga kudhalilisha na kutweza utu wa mtu bila kujali heshima, umri na nafasi yake katika jamii jambo ambalo halikuwahi kuwa utamaduni wa Watanzania.

"Hivi karibuni kumezuka tabia mpya ya watu badala ya Kujadiliana kwa hoja, kutoa mawazo yao au kukosoa Serikali kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18(1) inayotoa uhuru wa kila Mtanzania kujieleza. Badala yake wameanza kutukana matusi mazito kwa Watanzania wenzao na viongozi wao na wakubwa wao katika umri," alisema Matwebe,

Alisema vite do hivi ni kinyume kabisaa na Utamaduni wetu, mila zetu na desturi yetu kama Watanzania inayotutaka kuheshimiana sisi kwa sisi wadogo lakini pia kuheshimu watu waliotudizi umri. Jambo hili likiachwa linaweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu na kuleta maafa makubwa katika Jamii yetu au Nchi yetu.

Alipngeza kuwa siyo Viongozi wote wataweza kuvumilia kuona wao wanatukanwa au wazazi wao kutukanwa matusi mazito mbele ya hadahara, hivyo jambo hilo ni hatari na kama litaachwa liendelee kisha likaenea kwa Wananchi kuwa na utamaduni wa kutukanana wao kwa wao au Kutukana Viongozi wa Nchi kama utamaduni mpya wa Mtanzania inaweza kupoteza Amani ya Nchi.

Aidha ametumia mkutano huo kuwasihi Watanzania kuacha tabia hiyo isiyovumilika pamoja na kuacha kueneza matusi kusambaza matusi au kushiriki katika mijadala ya matusi.