Breaking News

RC CHALAMILA AUNGANA NA WAKAZI WA KINONDONI KATIKA DUA MAALUM YA KUOMBEA TAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila akizungumza katika dua maalum ya kuombea taifa wilaya ya kinondoni.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Saad Mtambule akizungumza katika dua maalum ya kuliombea taifa iliyoandaliwa na wilaya hiyo.

Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameungana na wakazi wa Wilaya Kinondoni katika ukumbi ulioko Soko la Magomeni kuomba Dua maalum kwa viongozi wakuu wa nchi na Taifa la Tanzania

RC Chalamila amesema Tanzania ni moja kati nchi chache Duniani ambazo Muungano wake ni wa mfano waasisi wa Taifa hili Hayati Mwl JK Nyerere na Hayati Amen Abeid Karume waliunganisha nchi hizi mbili Tanganyika na Zanzibar na kupata jina Tanzania, waliona umuhimu wakuliunganisha Taifa kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa.
Hivyo katika sherehe za miaka 60 ya Muungano Jamhuri ya Tanzania tunashudia mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali mfano wa kawaida ukiwa katika soko la karikoo wapemba ni wafanyabishara maarufu Alisema na kuongeza kuwa  

"tunapoadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanzania tumwombee kwa dhati Mhe Rais na Taifa kwa ujumla"

Aidha RC Chalamila amesema miundombinu mingi imeboreshwa ikiwemo mashule, masoko na barabara kinachotakiwa sasa kila mmoja kuulinda Muungano kwa nguvu zote kwa ustawi wa watu wetu katika pande zote mbili bara na visiwani