Breaking News

RC CHALAMILA UHARIBIFU WA BARABARA KUTOKANA NA MVUA SERIKALI HAIJALALA IKO IMARA

# Awatoa hofu wananchi DSM atoa taarifa kwa umma kuhusu ujenzi wa barabara lukuki katika Mkoa huo

Dar es Salaam:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 15,2024 akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake Ilala Boma amesema mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zimepelekea uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, Serikali haijalala iko imara hivi karibuni miundombinu hiyo itarekebishwa na kujengwa kwa kiwango cha lami.

RC Chalamila amesema kila wilaya barabara zitajengwa ikiwemo Ilala Km 55.27, Ubungo Km 54.27, Kigamboni Km 42.11, Temeke Km 52.71, na Kinondoni Km 48.33 ambapo ametoa rai kwa wakandarasi wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi nzuri waombe kazi hiyo mara tu itakapo tangazwa.

Aidha RC Chalamila aliongeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anadhamira ya dhati katika kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi katika nyanja anuai, hivyo amewaomba wananchi kuwa watulivu kutokana na kadhia wanayoipata ambayo imesababishwa na uhalibifu wa barabara katika maeneo yao kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.