BRELA YASHINDA TUZO YA TAASISI BORA KIDIGITALI
Afisa Habari Mkuu Bi. Christina Njovu kipokea Tuzo ya Taasisi bora ya Kidijitali kutoka kwa Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Mehdi Hussain katika hafla ya kutoa Tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Mehdi Hussain akizungumza katika hafla hiyo mara baada ya BRELA kutambulishwa kama Taasisi bora ya Serikali Kidigitali katika hafla ya kutoa Tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imepata tuzo katika kipengele cha taasisi bora ya Serikali kidigitali ikiwa ni kutambua mchango bora katika mageuzi ya kidigitali nchini Tanzania.
Tuzo hizo zimeandaliwa chini ya programu iitwayo Funguo Innovation inayosimamiwa na UNDP kwa kushirikiana na Kampuni ya Serengeti Bytes na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) yenye lengo la kutambua michango mbalimbali inayotolewa na Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi nchini katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Tuzo za Kidigitali kwa mwaka 2024 zilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya wiki ya ubunifu ikiangazia mafanikio na changamoto katika ubunifu wa kidigitali.






