Breaking News

JE WAJUA? KIWANDA PEKEE CHA KUUNGANISHA NDEGE EAC KIPO TZ

katika jitihada za Serikali za kukuza fursa za ajira na ukuzaji wa teknolojia (technological transfer) kwa wazawa, Serikali kupitia TAA imewezesha uwekezaji wa kiwanda cha uunganishaji na utengenezaji wa ndege ndogo katika Kiwanja cha Ndege cha Morogoro kupitia Kampuni ya Airplane Africa Limited.

Kampuni hiyo inafanya kazi ya kuunganisha na kutengeneza ndege za kubeba abiria wawili (2) ambazo ni aina ya “Skyleader”. 

Kwa sasa kiwanda hicho ni cha pekee Afrika Mashariki ambapo kina matawi katika nchi za Urusi, Jamhuri ya Czech, Ujerumani na China.