Breaking News

DKT SAMIA KAWEKA MAZINGIRA RAFIKI YAKUFANYIA BIASHARA (JWK)

 

Jumuiya ya wafanyabiashira Kariakoo (JWK) wamemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwawekea mazingira wezeshi yakufanyia biashara ikiwemo kuweka mifumo mizuri ya utozaji wa kodi.

Pongezi hizo zimetolewa leo Juni 7 2024 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Martin Mbwana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari nakufafanua kuwa kwa sasa wafanyabiashara hao wanafanya kazi zao katika mazingira mazuri licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo mfumo mbovu wa utoaji wa risiti za EFD.

Mbwana amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa kwa wafanyabiashira ambapo wamekutana na wizara zaidia ya tatu ikiwemo wizara ya fedha na Mipango,Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani nakufanya mazungumzo yanayochangia uboreshaji wa mazingira yao ya biashara.

" katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu kijaji aliwaahidi wafanyabiashira kuongeza bajeti ya wizara kwaajili ya kuboresha mazingira ya biashara,kuwakutanisha na TRA na kuweza kuangalia namna ya kupunguza utitiri wa kodi, amesema Mwenyekiti huyo wa JWK.

Nakuongeza kuwa " tumewaomba TRA wanapotekeleza majukumu yao wasijifiche,tushirikiane tufanye kazi kwa pamoja tujenge nchi yetu sote, wafanyabiashira tupo tayari kulipa kodi bila shuruti, hivyo ipende kutoa wito kwa TRA hata wanapoleta vijana wapya katika kukusanyakodi watutambulishe wasinifiche wakawa wanawawinda wafanyabiashira".

Aidha amebainisha baadhi ya Kero zinazoendelea wakabili wafanyabiashira hao kuwa ni pamoja na VAT ,namna ya uwasilishaji wa risit za EFD, na uingizaji wa mizigo kutoka nje.

Wafanyabiashira wanaomba kodi zote ziishie bandarini na si kuwafuata mara kwa mara katika maeneo yao ya biashara ili kuepusha mianya ya rushwa, kwasababu kuna vishoka wengi ambao wanajitokeza kuwasumbua wafanyabiashara wetu