Breaking News

DOYO HASSAN DOYO ATANGAZA RASMI KUWANIA UENYEKITI ADC TAIFA

Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Allience for Democratic Change (ADC), mheshimiwa Hamad Rashid kutangaza kung'atuka rasmi katika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba, katibu wa chama hicho bwana Doyo Hassan Doyo ametangaza rasmi Nia ya kuwania nafasi hiyo. 

Akizungumza mapema leo Juni 6, 2024 makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es Salaam amesema lengo la kuwania nafasi hiyo kwani anatosha kuchukua nafasi hiyo na atachukua fomu rasmi kuwania nafasi hiyo Juni 11 mwaka huu.

"Ninayo dhamira ya dhati pamoja na kuwa na uzoefu wa kutosha kufatia kuandaliwa vema na aliyekuwa Mwenyekiti Hamad Rashid ni moja sababu kubwa ambayo imenisukuma kugombea nafasi hiyo ni kutokana". Alisema bw. Doyo.

Alisema nimefanya kazi Mwenyekiti wa kwanza wa chama, Said Bilal nikiwa Mkurugenzi wa Habari na miaka zaidi ya 10 chini ya Mwenyekiti Hamad Rashid nikiwa kama Katibu Mkuu nimejifunza mengi ikiwemo suala uvumilivu na kuheshimu Katiba ya chama chetu, na kuitekeleza kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuachia madaraka kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea.

Amewataja wengine kuwa ni Lucas Silimu aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo, Mama Lydia Bendera (Katibu Mkuu), Juma Kilagai (Katibu Mkuu) na Abubakari Rakesh.

"Nichukue nafasi hii kuwatoa hofu wanachama wote wa chama hicho kutokuwa na wasiwasi na kuniunga mkono katika uchaguzi utakaofanyika Juni 27 jijini Dar es Salaam". Alisema Bw. Soyo.

Akizungumzia mipango yake mara baada ya baada kupata ridhaa ya kuongoza ambapo aliambatana na mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti, Bi. Scolastica Kahana aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2020 amesema ikiwa atachaguliwa kushika nafasi hiyo nitahakikisha nakiimarisha chama kuwa chama kikuu cha upinzani na kifanya vizuri bungeni kuisimamia Serikali Kwa maslahi ya Watanzania.

Ametaja mkakati mwingine kuwa ni pamoja na kuatabeba agenda tatu ambazo ni mabadiliko ya sheria, mabadiliko ya ajira ambayo itafanya wanafunzi kupata elimu Bora itakayowasaidia maishani na agenda ya maisha Bora kwa Mtanzania.