Breaking News

VIONGOZI WA DINI WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUFATIA MTANDAO WA KIJAMII WA "X " (TWITTER) KUHAMASISHA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Viongozi wa Dini nchini wametoa wito kwa Mamlaka za serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter Kwa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga)

Ombi hilo limetolewa leo Juni 11, 2024 Jijini Dar Es Salaam na Alhaj Dokta Abdul Suleiman wakati akizungumza na waandishi wa habari nakubainisha kwamba vitendo vya Mapenzi ya Jinsia Moja (Ushoga ) vimepigwa marufuku hata katika maandiko ya dini ya kiislam na kikristo ,hivyo vitendo hivyo havikubaliki na vinapaswa kulaaniwa mara moja.

Alisema Mtandao wa X ambao hapo zamani ulijulikana kama “Twitter” umeanza kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji Mamlaka zinazohusiana na mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ikiwemo kufuta mtandao huo hapa nchini.

Nae Askofu na Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Allen Siso amesema katika vitabu vya dini vyote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili,na wanaume nao vivyo hivyo'.

Kwa upande wake Sheikh Hilal Kipozeo amesema mtandao wa X unatakiwa kufutwa haraka iwezekanavyo,nakwamba ni vyema kuundwa Sheria kali ya Kudhibiti mapenzi ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.

“Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe". Alisema Sheikh Kipozeo.

Mapema Akizungumza mwakilishi wa walimu ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Gongo la mboto, Munira Njau amesema kuwa wazazi wamekuwa na tabia za kuwaachia watoto wao wachezee simu zao Hali iliyopelekea watoto kuingia kwenye mitandao hiyo na Kujifunza tabia mbaya siku Hadi siku na hatimaye kuzipeleka mashuleni.

"sisi walimu tunashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na tunakutana na wanafunzi ambao tayari Wana viashiria vya tatizo hilo na tunapowahoji wanasema wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao,hivyo suala hili tuungane wote kusaidia watoto.