WAHANGA MAPOROMOKO YA HANANG WASHUKURU SERIKALI
Na Mwandishi Wetu:
Waathirika wa maporomoko ya maji na tope katika kijiji cha Ganana wilayani Hanang mkoa Manyara wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada inazochukua katika kuhakikisha kuwa wanapatiwa huduma stahiki ikiwemo msaada na tiba ya kisaikolojia kwa baadhi ya wanafunzi waliopoteza wazazi ua walezi wao.
Wamesema kupitia misaada hiyo hususani tiba ya kisaikolojia imewasaidia hususani kwa wale waliopata Matatizo la athari ya afya ya akili kutokana na msongo wa mawazo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji hicho bwana Maiko Henda amesema kumekuwepo na changamoto ya wahanga wengi kupoteza mali pamoja na watehlgemeilzi wao (wazazi au walezi).
"Tumekuwa na changamoto kubwa hivi sasa ni wahanga wengi wengi kupoteza wazazi, ndugu na mali". Alisema Bw. Henda
Alisema Serikali imekuwa ikiendelea kuchukua jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za kijamii sambamba na kutuma timu za wataalamu wa tiba na saikolojia kutoka Wizara ya Afya na Tamisemi kufanya tathimini ya athari zilizojitokeza pamoja na utoaji wa elimu kuhusu masuala mbalimbali kwa waathirika hao.





