WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA KITAIFA WA RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA SAMBAMBA NA KUMBUKIZI YA HAYATI BENJAMIN MKAPA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasili katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiambatana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui wakimsikiliza mkurugenzi wa hospital ya Muhimbili Profesa Mohammed Janabi katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.
Dar es Salaam:
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa atafungua Mkutano wa kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Afya sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Benjamin Mkapa, leo Julai 30, 2024.
Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Kaulimbiu ya Mkutano huo ni “Nguvukazi Sekta ya Afya: Mhimili wa Maendeleo Endelevu”. Kaulimbiu hii imebeba uhalisia wa masuala muhimu kwa mandeleo endelevu ya sekta ya afya.







