Breaking News

BAWACHA WALAANI TUKIO LA UNYANYASAJI WA JINSIA KUFATIA KUSAMBAA VIDEO TUKIO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Na Neema Mpaka
Baraza la wanawake wa chama cha Demokrasi na Maendeleo (BAWACHA) wamelaani tukio la uzalilishaji na unyanyasaji kufatia kusambaa video katika mitandao ya kijamii na kumtaka rais Samia Hassan kutoa kauli juu ya kitendo hicho.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa bawacha mkoa wa kinondoni, Bi. mariamu rashidi Makala amesema tukio hilo ni la uzalilishaji huo sio tu limdhalilisha aliefanyiwa bali limedhalilisha wanawake wote tuanaiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wahutumiwa hao.
Aidha Bi mariamu amelisihi jeshi la polisi kuchukua hatua haraka hatua za kisheria kutokana na wahutumiwa wote wa tukio hilo Zima wameonekana na sio kusubiri uchunguzi wakat tukio lote liko wazi.

"Tunalitaka jeshi la polisi nchini kuchukua hatua haraka kwa wahusika wote wa tukio hilo kwani watuhumiwa wote wanaonekana katika video ya tukio hivyo taarifa ya kwamba wanafanya uchunguzi aikubaliki kwani kuongeza tu sintofahamu katika jamii". Alisema Bi. Makala.

Alisema kufatia tukio hili Bawacha tunapenda kutoa rai kwa heshi la polisi nchini kuja na majibu kamili ya tukio husika na hatua zitakazo chukuliwa sambamba na matukio ya kuhusiana na utekaji wa watoto na watu wazima.

Katika htua nyingine Bi Makala amewataka wanawake wote ambao wamekutana na matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kujitokeza na kutoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria ili wahusika kuchukuliwa hatua Kali zichukulie kwa watuhumiwa