Breaking News

JAMII BADO HAINA UELEWA JUU YA UGONJWA WA KIFAFA

Mratibu afya ya akili kutoka manispaa ya kinondoni, Dokta Peter Mwendo akwasilish mada katika warsha ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya maradhi ya kifafa jijini Dar es salaam.
Shujaa wa ugonjwa wa kifafa bi. Isrey Ayub akifafanua jambo katika warsha ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya maradhi ya kifafa jijini Dar es salaam. 

Dar es salaam:
Jamii imetakiwa kutokuwatenga wagonjwa wa kifafa kwani hata wao wanao uwezo na haki ya kupata huduma zote muhimu ikiwemo elimu. 

Dkt. Mwendo amesema hayo katika kikao kilichoandaliwa na Taasisi ya wazazi wa watoto wenye kifafa (UWAKITA). ambacho kilihudhuriwa na wadau wake ikiwamo Taasisi ya Waandishi wa Habari za Afya ya Akili Tanzania (TAMHJO) na waratibu wa Afya ya Akili kutoka maeneo mbalimbali nchini.
"Elimu hii inatakiwa kutolewa kwa jamii kwa ujumla katika jamii kuna mifumo ya afya ngazi ya jamii wakishapata elimu ya kutosha kuhusiana na kifafa wanaweza kusaidia na wananchi wengine kuwaeleza juu ya ugonjwa huo hivyo kutokomeza unyanyapaa katika jamii" Alisema Dkt. Mwendo

Alisema elimu hii pia itolewe elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa nao kuwa na ufahamu mzuri juu ya ugonjwa wa kifafa hili nao lusaidia kutoa elimu kwa wananchi katika maeneno yao juu ya ungonjwa huu.

Aidha Dkt Mwendo aliongeza kuwa elimu ya kutosha itolewe pia kwa watoa huduma ya afya kwani wao wanao ushawishi kubwa katika jamii hivyo kupitia wao wanaweza kusaidia jamii kupata ufahamu mzuri zaidi juu ya ugonjwa wa kifafa.
Dkt. Mwendo amesema ni vizuri serikali na watoa huduma wakatambua kwamba jamii ikipata elimu kuanzia ngazi ya zahanati ni nzuri zaidi kwani wanapata elimu hiyo mapema kuliko kuanza tena kufikilia kwenda katika hospital kubwa.

"Nitoe rai kwa serikali kutambua kwamba jamii ikipata elimu ya kifafa katika ngazi ya zahana7ni ziri zaidi kuliko kuanza kufikilia kwenda hospital ya Muhimbili au hospital nyingine kubwa kupata elimu hiyo". Alisema.