Breaking News

MGOMBEA UBUNGE UKONGA JERY SILAA AMESEMA MIKAKATI YAKE UKONGA KUWA YA KISASA

Na Heri Shaaban (Dar es Salaam) - Mhombea wa Ubunge Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala Mkoa Dar es Salaam Jery Silaa,aeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi utakavyolibadirisha jimbo la Ukonga kuwa la kisasa .

Mgombea Ubunge Jery Silaa, alisema hayo katika uzinduzi wa kampeni za jimbo la Ukonga mkoa Dar es Salaam ambapo katika uzinduzi huo warishiriki na wagombea udiwani saba wa jimbo hilo kuomba ridhaa kwa wananchi ili wawachague.

"Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM wakati nikiwa mbunge wa jimbo la ukonga kabla kugawa kata 13 mpaka kubaki kata saba awali Jimbo la Ukonga lilinizidi ukubwa chupu chupu liniue lakini kwa sasa nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuligawa jimbo hii"alisema Jerry 

Jerry alisema katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi alivyosimamia wakati uliopita Kata ya Pugu Bangulo sekta ya maji tanki kubwa Rais amefunga maji kwa sasa maji hayo yanalisha Pugu Bangulo,Gongolamboto,Kitunda,mpaka jimbo la Kivule ni kazi kubwa ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kufunga tanki kubwa la maji kuwatua ndoo kichwani kina mama aliomba wananchi wa jimbo hilo kumpa zawadi Dkt.Samia kura zote za Urais .

Aidha alisema mengine aliyotekeleza utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi akiwa Meya wa wa Manispaa ya Ilala na Mbunge wa Jimbo la Ukonga ameweza kujenga hospitali ya Mama na Mtoto nguvu kazi Chanika ,ameweza kujenga Kituo cha afya Zingiziwa,Buyuni,Mvuti,Pugu Station ,Mzinga Kituo cha afya golofa mbili Shilingi bilioni 9 zilitumika ,Mikongeni Kituo cha afya Gongolamboto na Jengo la Macho katika Hospitali ya Wilaya kivule  

Akizungumzia sekta elimu Dkt samia suluhu Hassan toka aingie madarakani akuna mzazi anatozwa pesa shule za kisasa zimejengwa Nyeburu,Kigezi chini,Yongwe,na shule za Sekondari Ukonga ya golofa mbili,Nguvu mpya,Zogoali,Gulukwa kwalala,Barabara njia sita Mwendokasi Gongolamboto Kariakoo Mpaka posta na Umeme nishati ya umeme inapatikana kwa asilimia 100 kwa wananchi wote.

Akizungumzia mikakati yake akiingia madarakani kubadirisha Jimbo la Ukonga kuwa la kisasa kwa kujenga masoko ya kisasa Gongolamboto ,Zingiziwa,Chanika ili kuwapangia utaratibu Wajasiriamali katika fursa za kiuchumi waweze kukuza uchumi wa nchi yao.

Kwa upande mwingine aliwataka wagombea udiwani wa jimbo la Ukonga wakichaguliwa na wananchi wakaanze kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo vizuri ambayo Rais Dkt.Samia aemelekeza fedha pamoja na mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri ili kila mwanachi aweze kupata mikopo hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema mpaka sasa CCM Wilaya ya Ilala kata nane wamepita bila kupingwa wanasubiri kupigiwa kura za ndio au hapana kwa wagombea wa kata hizo.

Mgombea ubunge Jimbo la Kivule Wilayani Ojambi Masaburi aliwataka wananchi wa jimbo la ukonga kumchagua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Madiwani wa Ukonga pamoja na Jery Silaa, sababu amefanya mambo makubwa akiwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na sasa ni Waziri wa Habari na Mawasiliano