Breaking News

TBS: USINUNUE BIDHAA HIZI 106, TUMEZISITISHIA LESENI YA UBORA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuutaarifu umma kuwa limesitisha vyeti na leseni 106 za kutumia alama ya ubora ya TBS kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maombi ya kufunga biashara na kutokutii masharti ya leseni kwa mujibu wa Kanuni ya 28 ya Kanuni za Usajili wa Majengo na Uthibitishaji wa bidhaa, 2021 (The Standards (Registration of Premises and Certification of Products) Regulations, 2021).

TBS inauasa Umma kuepuka kununua au kusambaza bidhaa zilizositishiwa kutumia alama ya ubora ya TBS na kutoa taarifa endapo watabaini bidhaa hizo zipo sokoni.

Orodha kamili ya vyeti na leseni zilizositishwa