Breaking News

RIDHWANI AWAFUNDA WADAU MIFUKO YA JAMII

Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikiia Utumishi na Menejimnti mh.Ridiwani Kikwete (katikati) waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria mkutano wa kujadili uimarishaji huduma za mifuko ya jamii mjini Arusha juzi.( Picha na Rajabu Shareef)


Arusha - Watanzania wanaojiajiri sekta binafsi wameshauriwa kujiunga na mfuko ya wa kinga ya jamii ambao una faida kubwa katika maendeleo ya shughuli zao.

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais Utumishi na Menejienti mhe. Ridhuwan Kikwete alitoa ushauri huo juzi mjini Arusha wakati akifunga mkutano wa wadau wa kinga ya jamii.

Alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha dhamira njema ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuongeza wigo wa huduma ya kinga kwa wananchi hasa waliojiajiri kwenye sekta isiyo rasmi.

"Kwa muktadha huo nawasihi watanzania wasiache fursa ya kushiriki kwenye huduma za hifadhi ya mifuko ya hifadhi hizo hasa inapoanza kutumika sera mpya nchini pote".alielekeza waziri Ridhwani.

Hii ni katika kutimiza ahadi ya Rais Samia ya kukamilisha mambo kadha yanayogusa umma ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani Novemba 2025.