SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA KUFUATILIA CHANGAMOTO
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais bwana Ridhwani Kikwete ( kushoto) anazindua vifaa vya mfumo wa kutoa mrejesho kuhusu majukumu ya watumishi wa umma kwenye hafla iliyofanyika Chalinze mkoani Pwani juzi. ( Picha na Rajabu Shareef)
Na Mwandishi Wetu - Wizara ya Utumishi Menejiment na utawala bora imezindua rasmi mfumo mpya uitwao e-mrejesho ili kupata taarifa sahihi za ufuatiliaji wa changamoto zinazokabili wananchi na taasisi za umma nchini.
Mfumo huo uliobuniwa na vijana wa Kitanzania ulitambulishwa rasmi jana na waziri wa nchi ofisi ya Rais bwana Ridhwani Kikwete huko Chalinze mkoani Pwani kwenye hafla iliyphudhuriwa na wananchi kutoka sehemu kadha.
Katika hafla hiyo ya kutambulisha mfumo mpya waziri Kikwete alisema utawezesha Watanzania kukutanishwa na viongozi hasa watumishi wa umma ili kujua utekelezaji wa malengo unavyoendelea katika ngazi mbali mbali.
Wakati huo huo serikali imetps gari la zimamoto na gari la ambulensi lwa ajoli ya huduma za wananchi jimbo la Chalinze na maeneo ya jirani ii kukabili matatizo yanayotokana na uhaba wa vifaa vya tiba na huduma zingine.




