Breaking News

PICHA: BRELA YATOA TUZO KWA WADAU MBALIMBALI WA MICHEZO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga akitoa tuzo kwa Prof Saudin Jacob Mwakaje Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Wakili wa Mahakamu Kuu akiwa na mchango wa Kitaalamu kwenye kukuza na kuendeleza nyanja ya Miliki Ubunifu nchini. Prof Mwakaje ni miongozi mwa waanzilishi na mratibu wa programu ya Shahada ya Miliki Ubunifu (MIP) inayotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na BRELA, WIPO na ARIPO ili kuongeza wataalam wa Miliki Ubunifu nchini
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa tuzo kwa mwanariadha Alphonce Simbu akiwa ni mwanamichezo aliyetangaza Tanzania Kimataifa (National Branding)
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa tuzo kwa mchezaji wa Kikakpu Hasheem Thabeet akiwa ni mwanamichezo aliyetangaza Tanzania Kimataifa (National Branding). Tuzo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi akitoa Tuzo kwa Imanuel Mlefu Nakalu mchezaji wa mpira wa miguu mwenye ulemavu ambaye ameshiriki na kuisaidia Tanzania kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa wachezaji wa mpira wa miguu wenye ulemavu pia amekuwa mchezaji bora wa mashindano ya Azam Amputee Football Tournament.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi akitoa Tuzo kwa Rehema Said Selemani mwanamichezo mwenye ulemavu na aliye na mchango mkubwa katika ukuaji wa michezo nchini. Bi Rehema Selemani anamafanikio katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kikanda hususan mashindano ya Shirikisho la Tenisi Duniani kwa wachezaji wa viti mwendo.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa tuzo kwa taasisi za fedha inayotumia Miliki Ubunifu na imechangia kukua kwa sekta ya michezo kwa mwaka 2025/2026. Taasisi hizo ni Benki ya CRDB na Benki ya NBC.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi akitoa kwa Kampuni ya Sigara Tanzania ikiwa ni Kampuni ya Kwanza Tanzania kusajili Alama ya Biashara ya nchini mwaka 1962 kwa Bidhaa ya Sweet Menthol (SM)
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga akitoa tuzo kwa mwanamke mjasiriamali Mwilongo Ngobolipemba Semapembe anayetumia Alama ya Biashara
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga akitoa tuzo kwa mwanamke mbunifu bora Never Daudi Zekeya. Bi Zekeya amebuni teknolojia ya uzalishaji wa vichocheo hai vya mimea viuatilifu vya kudhibiti wadudu

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa tuzo kwa vilabu vinne vya Michezo zilizosajili Alama ya Biashara na kutumia Miliki Ubunifu.Vilabu hivyo ni Yanga, Simba, Mbeya City na Azam Football Club.