DC MWAIPAYA AWAALIKA WATANZANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA NYANGUMI MNAZI BAY
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, amewataka wananchi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kushiriki Tamasha la Nyangumi linalotarajiwa kuanza kesho na kuhitimishwa Septemba 5, mwaka huu.
Mwaipaya amesema tamasha hilo hufanyika kila mwaka kutokana na uwepo wa kivutio cha nyangumi wanaofika katika maeneo ya bahari ya Mtwara katika ghuba ya Mnazi Bay kijiji cha Msimbati kwa ajili ya shughuli zao za kawaida ikiwemo kuzaa.
Amesema tamasha hilo ni fursa kwa wananchi na wageni kutoka maeneo mbalimbali kujifunza, kutembelea maeneo yenye Nyangumi na kutambua umuhimu wa uhifadhi wa bahari na rasilimali zake.
Mwaipaya amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika kipindi chote cha tamasha hilo.
Mkurugenzi wa hifadhi ya mnazi bay Redfrey Ngowo amesema licha ya kivutio hiko,katika hifadhi hiyo vipo vivutio vingine ikiwemo milima ya mchanga ,maingilio ya mto Ruvuma samaki mbalimbali akiwemo Pomboo pamoja na fukwe nzuri pamoja na matumbawe
Amesema tamasha hilo limekuwa la kipekee kwan washiriki wamekuwa wakijionea vivutio hivyo pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali za kiuchumi




